Wito wa kuudhuria tarehe 25 Mai

Ubaguzi wa rangi na Unyanyasaji wa Polisi kwa wananchi usimame mara moja!

Tunaandaa na kuposha shuguli mbali mbali zinazozunguka ikiwemo tamasha mnamo 25 Mai 2021

…Mwaka mmoja tangu George Floyd auwawe kikatili tarehe 25 Mai 2020

…Siku  hii ikiwa pia ni siku ya kumbukumbu ukombozi wa Afrika (ALD), ambayo ilikuwa siku ya muungano wa wafrika dhidi ya Utawala wa kikoloni tarehe 25 Mai 1963

…Miaka kumi sasa tangu Christy Schwundeck auwawe kikatili tarehe 19 Mai 2011.

 
Kwetu sisi kupambana na ubaguzi wa rangi siyo mwenendo au hobby, bali mapambano ya kila siku. Kwetu sisi siyo tangu kifo cha kikatili cha George Floyd. Iwe katika Makrekani, Brasil, Haiti, Nigeria, Senegal au hapa Ujerumani, mahali popote pale ni muhimu kujilinda na kuungana kwa pamoja. Ifahamike kwamba Tarehe 25 Mai siyo tu siku ya George Floyd kuuwawa. Tangu mwaka 1963 tarehe 25 Mai ni siku ya ukombozi wa Akfrika (African Liberation Day) ambayo inasherekewa katika bara la Afrika na diaspora ya waafrika. Siku hii inaonyesha amuzi yetu kuungana na kujikomboa kutoka kila aina ya utawala ya kigeni.
 
Dunia ya sasa na Uchumi wake kiujumla imeegemea kwenye utumwa wa kizungu, ikiwemo kumwagika kwa damu ya watu wengi na ukoloni. Ubaguzi wa rangi unatumika kama chombo cha madharau bila mwisho na dhuluma. Mauaji ya kupangwa, dharau, udhalimu na kuvunjwa moyo wa watu Weusi katika Afrika na dunia nzima inaeleweka tu njee ya pazia.
 
Mwanzo wa ubaguzi wa rangi katika nchi ya Ujerumani haujaanza kipindi cha utawala wa kibaguzi (Nazi-Regime). Uchuma wa Ujerumani ni muendelezo katika faida za utumwa, mauaji ya halaiki Namibia na pia maafa ufashisti yanayo andaliwa kiserekali. Ujerumani inshashirikia katika usafirishaji wa silaha, vita, matusi katika kambi za wahamiaji na vifo vya watu wengi katika bahari ya kati.
 
Polisi kuwauwa watu kwa ajili ya ugabuzi wa rangi siyo kitu cha nadra. Katika mauaji maharufu ni kifo cha John Achidi na N’deye Mareame Sarr mwaka 2001 vilevile Oury Jalloh na Laya-Alama Condé mwaka 2005. Mwaka huu ni miaka kumi tangu Christy Schwundeck auwawe. Tarehe 19 Mai mwaka 2011 alipigwa risasi na polisi akiwa kwenye Jobcenter Gallus kule Frankfurt am Main.
 
Unyanyasaji wa ubaguzi wa rangi hayaanzi tu pale polisi wakitukimbiza na kutuuwa. Iwe katika sheria, makao na makazi, afya, elimu, utamaduni na mida huru: Ni mfumo mzima ambao unatunyanyasa katika kila idara na kila sehemu ya maisha.
 
Serekali ya Ujerumani, vyama na NGOs zimeshaonyesha kwamba hazina uwezo wa kuendeleza masilahi yetu. Ndiyo maana tunawaalika wote, ili kujipanga na kuwa na maisha ya pamoja bila kuwepo aina yoyote ya ubaguzi wa rangi pia kutokutumiwa, dhuluma na udhalimu.
 
Tunasimama kwa ajili ya ukombozi wa watu Weusi wote. Bila kujali popote pale tunapoishi tumeunganika na muungu wa pamoja, historia ya pamoja iliyoanza Afrika. Ikiwa bado bara la Afrika imefungwa na mnyororo hakuna mtu mweusi atakayoishi katika uhuru wa kweli. Kwa sababu hiyo tunachukuwa nafasi hii kutokomeza dhaluma na utumwa wa kutumiwa na vita kubwa kubwa inayo endelea dhidi ya bara la Afrika.
 
Ni kwa muungano na kua pamoja ndio tutatua wenye nguvu!
Tujiunge pamoja na kujikinga!
 
„Ni wajibu wetu sote kupambana kwa ajili ya uhuru wetu. Kwetu sisi ushindi ni lazima. Lazima tuwe na upendo na tusaidiane kwa hali na mali.” – Assata Shakur